Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imesema kuwa mapambano ya wananchi wa Yemen yanalenga kurejesha haki zao halali na kumaliza mzingiro unaoikabili nchi hiyo, huku ikisisitiza kuwa hakuna nguvu yoyote itakayoweza kuwazuia kufikia malengo hayo.
Katika taarifa yake, wizara hiyo ilieleza kuwa utawala wa Saudi Arabia uko katika hali ya mkwamo wa kihistoria, na kuvitaka mataifa ya dunia kutodanganywa na kile ilichokiita vita visivyo na mafanikio vinavyoendelea dhidi ya Yemen.
Wizara hiyo pia ilionya kuwa uwepo wa majeshi ya kigeni katika Bahari Nyekundu unaweza kusababisha hali ya kutokuwa na utulivu na kuathiri usalama wa shughuli za usafiri wa majini. Aidha, ilisisitiza kuwa njia ya Bab al-Mandab pamoja na Bahari Nyekundu ni salama, na kwamba taarifa zozote zinazodai kuwepo kwa hatari au vikwazo katika eneo hilo hazina ukweli.
Mwisho, Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen ilisisitiza kuwa hata kama mataifa yote duniani yangeungana kuzuia wananchi wa Yemen kupata haki zao za kisheria, juhudi hizo zingeshindwa. Pia ilieleza kuwa hatua za kuondoa mzingiro uliowekwa na Saudi Arabia na kurejesha haki kamili za wananchi wa Yemen bado zinaendelea na ziko katika hatua za awali.
Maoni yako